The United Republic of Tanzania

TANZANIA INVESTMENT CENTRE

Mdahalo wa kusikiliza changamoto za Wawekezaji ni hatua ya kutafuta ufumbuzi wa kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini.


 

17 Aprili,2019: Mhe. Angellah Kairuki amekuwa Mgeni rasmi na Mwenyekiti kwenye mdahalo wa wawekezaji wa Kichina waliowekeza nchini. Mdahalo huo umefanyika Serena Hotel, Dar es Salaam na pia umehudhuriwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Inj. Stella Manyanya (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Damas Ndumbaro (Mb), Balozi China nchini Mhe. Wang Ke na Wakuu/ Wawakilishi wa Taasisi za Serikali zipatazo ishirini (20).

 

Lengo la mdahalo lilikuwa ni kusikiliza changamoto za biashara na uwekezaji kutoka kwa Wachina waliowekeza nchini ili kuzitolea majibu na ufafanuzi. Aidha mdahalo pia ulilenga kutoa elimu/ kuwakumbusha wawekezaji wa Kichina njia sahihi za kufuata na nyaraka za kuwasilisha wanapoomba kupata huduma husika ili waweze kupata vibali, leseni na vyeti vinavyohitajika kufanikisha uwekezaji wao hapa nchini....

2019-04-18 17:08:43Mdahalo wa kusikiliza changamoto za Wawekezaji ni hatua ya kutafuta ufumbuziwa kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini.


17 Aprili,2019: Mhe. Angellah Kairuki, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -Uwekezaji amekuwa Mgeni rasmi na Mwenyekiti kwenye mdahalo wa wawekezaji wa Kichina waliowekeza nchini. Mdahalo huo umefanyika Serena Hotel, Dar es Salaam na pia umehudhuriwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Inj. Stella Manyanya (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Damas Ndumbaro (Mb), Balozi China nchini Mhe. Wang Ke na Wakuu/ Wawakilishi wa Taasisi za Serikali zipatazo ishirini (20).

 

Lengo la mdahalo lilikuwa ni kusikiliza changamoto za biashara na uwekezaji kutoka kwa Wachina waliowekeza nchini ili kuzitolea majibu na ufafanuzi. Aidha mdahalo pia ulilenga kutoa elimu/ kuwakumbusha wawekezaji wa Kichina njia sahihi za kufuata na nyaraka za kuwasilisha wanapoomba kupata huduma husika ili waweze kupata vibali, leseni na....

2019-04-18 17:01:31“Uchumi wa uwekezaji kwenye mifuko mbadala ni mkubwa kuliko uchumi unaotokana na uwekezaji kwenye mifuko ya plastiki” – Mhe. J. Y Makamba (MB)


‘Kwa mujibu wa Kanuni za Sheria ya Mazingira, Serikali imetoa tamko la katazo la mifuko ya plastiki nchini kunzia kwenye kuzalisha, kuuza ndani na nje ya nchi, kuingiza nchini kutoka nje ya nchi, kumiliki, kuhifadhi, na kutumia. Atakayekiuka Sheria hiyo, atapata adhabu.’

 

Ni ujumbe mzito uliotolewa kwa Wananchi kupitia kikao cha wadau  kilichofanyika tarehe 15 Aprili, 2019 kuhusu fursa za uwekezaji katika uzalishaji wa mifuko mbadala ya plastiki kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Lengo la kikao lilikuwa ni kuhamasisha Wadau kuhusu uzalishaji wa mifuko mbadala wa mifuko ya plastiki ili kuhifadhi mazingira. Kipekee kabisa kikao hicho   kilihudhuriwa na Waheshimiwa Mawaziri watatu ambao ni  Mhe. Angellah J. Kairuki, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji;  Mhe. Joseph Kakunda, Waziri wa Viwanda na Biashara  na....

2019-04-16 16:34:30Uchumi wa uwekezaji kwenye mifuko mbadala ni mkubwa kuliko uchumi unaotokana na uwekezaji kwenye mifuko ya plastiki’


 ‘Kwa mujibu wa Kanuni za Sheria ya Mazingira, Serikali imetoa tamko la katazo la mifuko ya plastiki nchini kunzia kwenye kuzalisha, kuuza ndani na nje ya nchi, kuingiza nchini kutoka nje ya nchi, kumiliki, kuhifadhi, na kutumia. Atakayekiuka Sheria hiyo, atapata adhabu.’

 

Ujumbe huo umetolewa kwa Wananchi kupitia kikao cha wadau  kilichofanyika tarehe 15 Aprili, 2019 kuhusu fursa za uwekezaji katika uzalishaji wa mifuko mbadala ya plastiki kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Lengo la kikao lilikuwa ni kuhamasisha Wadau kuhusu uzalishaji wa mifuko mbadala wa mifuko ya plastiki ili kuhifadhi mazingira. Kipekee kabisa kikao hicho   kilihudhuriwa na Waheshimiwa Mawaziri watatu ambao ni  Mhe. Angellah J. Kairuki, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji;  Mhe. Joseph Kakunda, Waziri wa Viwanda na Biashara  na Mhe.....

2019-04-16 16:30:38Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Kibiashara 'Tanganyika Business Summit & Festival’ litafanyika Mkoani Kigoma tarehe 9 - 11 Mei, 2019 katika ukumbi wa mikutano wa NSSF.


Ndugu Wadau wa Biashara na Uwekezaji nchini;

 

Mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Local Investment Climate (LIC), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Baraza la Biashara Tanzania (TNBC), Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA),Kigoma Joint Programm(KJP),International Trade Centre (ITC) na Afro Premiere kwa pamoja wanaandaa 'Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Kibiashara' maarufu kama 'Tanganyika Business Summit & Festival’. Kongamano hilo la aina yake litafanyika kwa siku tatu Mkoani Kigoma kuanzia tarehe 9 mpaka tarehe 11 Mei, 2019 katika ukumbi wa mikutano wa NSSF. Mgeni rasmi atakuwa ni Mhe.Samia S. Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Pamoja na mambo mengine, kongamano lina lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara wa Mkoa....

2019-04-08 11:49:56
Social Medias

Copyright ©2018 Tanzania Investment Centre.
All Rights Reserved.
Designed, Developed, and Maintained by Tanzania Investment Centre(TIC)