The United Republic of Tanzania

TANZANIA INVESTMENT CENTRE

Viongozi wamesikiliza, wamejibu, wameshauri na wameelimisha wafanyabiashra na wawekezaji Mikoa ya Kusini .


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Angellah Kairuki ameongoza ziara ya pamoja ya viongozi katika Mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara kati ya tarehe 23-27 Septemba, 2019. Ziara hiyo iliandaliwa pamoja na mikutano ya siku moja kati ya wawekezaji wafanyabiashara na viongozi. Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kushiriki mikutano ya mashauriano kati ya Serikali na wafanyabiashara na wawekezaji katika ngazi za Mikoa ili kuibua kero/changamoto na kupatiwa majibu kutoka kwa viongozi husika wa Wizara, Taasisi na Mamlaka wanazosimamia. Kero na changamoto za biashara na uwekezaji katika maeneo ya ardhi, kodi, mazingira, nishati, maji, ardhi viliwasilishwa na kupatiwa majibu. Vilevile viongozi walitumia nafasi hiyo kutoa elimu kwa umma kuhusiana na Ofisi zao na jitihada zinazochukuliwa na Serikali katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji. Aidha elimu juu ya umuhimu wa wawekezaji na wafanyabiashara kuendesha miradi yao ya biashara na uwekezaji kwa ukaribu na ofisi zinazotakiwa kufanikisha uwekezaji wao katika kila hatua pia limesisitizwa.

 

 

Viongozi wengine walioshiriki ziara hiyo ni Waziri wa Viwanda na Masoko Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko, Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Ashatu Kijaju, Naibu Waziri wa Nyumba Ardhi na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angelina Mabula, Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mussa Sima, na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde. Vilevile Wakuu wa Mikoa,  Wakuu na Wawakilishi wa Taasisi za Umma pia walishiriki. Kipekee kabisa wakati wa ziara hiyo, viongozi wote pamoja na mambo mengine, wamezungumza hatua zinazochukuliwa na Serikali kuboresha huduma kwa wawekezaji na umuhimu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) katika kufanikishwa uwekezaji wa wawekezaji watarajiwa nchini. 

 

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Angellah Kairuki amesema kwa sasa wanafanya maboresho yanayolenga kuja na Sheria Mpya ya Uwekezaji sambamba na kuboresha  Sheria ya Uwekezaji. Sheria na Sera vinalenga kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji na pia kuweka nafasi ya kuvutia na kuwezesha wawekezaji wengi. Akiyataja baadhi ya matarajio hayo ni kwamba mabadiliko ya sheria ya uwekezaji yanalenga kuvutia uwekezaji zaidi na itasaidia kupunguza kiwango kinachotakiwa ili kujisajili na TIC." Usajili utawasaidia kunufaika na faida zinazotokana na kujisajili ikiwamo vivutio vya kikodi na visivyo vya kikodi,"amesema Waziri Kairuki na kuongeza wanategemea mapendekezo hayo yawasilishwe Bungeni Novemba, mwaka 2019. Aidha, Mhe. Kairuki ameendelea kukemea matamko mabaya ya viongozi na vitisho kwa wawekezaji na wafanyabiashara, badala yake busara itumike katika kila hatua. Serikali ipo kwa ajili ya kuhudumia na kufanikisha malengo ya wafanyabiashara na wawekezaji kwa kuwa ndio wanatoa fedha ya maendeleo ya nchi amesema Waziri Kairuki. 

 

 

Naye Mhe. Innocent Bashungwa amesisitiza kwamba wetu unaendeshwa na sekta binafsi, hivyo watumishi wote wa Umma tusiwapape frustration wafanyabiashara na wawekezaji wetu badala yake tuwe facilitator kwao. Kwa kufanya hivyo watakuwa mabalozi wetu wazuri kwa wawekezaji wanaofikiria kuja kuwekeza Tanzania sambamba na kufanya biashara.

 

 

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabulla, amesema wawekezaji wote wanaohitaji ardhi lazima wapite TIC hasa wawekezaji wa kigeni ambapo pamoja na mambo mengine wanatengenezwa hati pacha ya umiliki yaani 'Deriverrive Right'. Hati pacha itampa mwekezaji uwezo wa kuimiliki ardhi yake kwa uwekezaji. Mhe. Mabulla kipekee kabisa ametoa wito wa Halmashauri zote kuhimiza wawekezaji wote hasa wa kigeni wanaohitaji ardhi ya uwekezaji kupitia TIC.  "Mnapopata ardhi kwa ajili ya uwekezaji msimpe mwekezaji moja kwa moja bali fuateni taratibu na sheria za kupitia TIC ili kujiepusha na migogoro inayoweza kujitokeza pasipo na sababu. Amesema lengo ni kutengenezewa hati pacha ya umiliki yaani 'Deriverrive Right' itakayompa uwezo wa kuimiliki Hili lizingatiwe,"amesema. Hata hivyo amesema Novemba 19 mwaka huu Wizara itafungua ofisi kila mkoa ili kurahisisha upatiknaji wa ardhi ikiwamo ya uwekezaji, upimaji na upatikanaji wa hati  katika ngazi ya kila Mkoa. Amesema hiyo itapunguza usumbufu kwa wawekezaji na wafanyabiashara kufuatilia hati mikoa jirani (Kanda) au Dar es Salaam. 

 

Wakati huo huo Naibu Waziri wa Fedha Dk.Ashatu Kijaji amesema hakuna nchi inayoendelea bila wafanyabiashara na wawekezaji. Na ili nchi iendelee tunahitaji kodi kwa maendeleo. Kodi inatokana na wafanyabiashara na wawekezaji hivyo tushirikiane nao vizuri. "Katika kuboresha na kuweka mazingira mazuri mwa wafanyabiashara na mwekezaji imeshauriwa wapewe miezi sita (6) kabla ya kuanza kulipa kodi baada ya kuanza utekelezaji wa miradi yao,"amesema.  Ameongeza kuwa hiyo itawapa muda wa kujifunza, kujitathmini na kujipanga kwa ajili ya kulipa kodi na kuongeza malipo yafanyike kupitia mashine za EFD zinazotolewa na TRA na sio vinginevyo. Pia amesisitiza kodi kulipwa kwa utaratibu wa sheria husika na si vinginevyo, hivyo maofisa wazingatie hilo na wafuate sheria wanapokusanya kodi. 

 

 

Kwa upande wa Wizara ya Mazingira, Naibu Waziri ameeleza kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya uwekezaji na mazingira na kwamba uwekezaji wowote unaofanyika lazima uwe endelevu (uzingatie sheria za kutunza na kuhifadhi mazingira) kwa matumizi ya leo na hata vizazi vinavyokuja. Wizara hiyo imetoa mwito kwa wawekezaji wote kuwasiliana na NEMC ama Afisa wake aliyepo TIC ili kupata miongozo ya mazingira na gharama mbalimbali ambazo kwa sasa zimepunguzwa. Hatua hiyo imefuatiwa ili kumpunguzia m,wekezaji mzigo wa gharama.

 

Katika ziara hii TIC iliwakilishwa na Mkurugenzi wa Utafiti, Mipango na Mifumo ya Tehama Bw.  Mafutah Bunini. Shukrani za pekee ziwafikieviongozi wote walioshiriki ziara hii kwa lengo la kufanikisha uwekezaji zaidi kwa maendeleo ya Taifa letu. Aidha ziara pia imeleta mwamko na imani kubwa kwa wawekezaji na ni imani kwamba kufuatia ziara hiyo, mwamko mkubwa wa uwekezaji utaoneka.Ziara kama hizi zitaendelea pia kwa Mikoa mingine.

Social Medias

Copyright ©2018 Tanzania Investment Centre.
All Rights Reserved.
Designed, Developed, and Maintained by Tanzania Investment Centre(TIC)