The United Republic of Tanzania

TANZANIA INVESTMENT CENTRE

Kituo cha Uwekezaji Tanzania Kanda ya Ziwa chini ya uongozi wa Meneja Bw. Fanuel Lukwaro kimepata ushindi wa kishindo .


Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Ziwa chini ya uongozi wa Meneja Bw. Fanuel Lukwaro kimeng’ara baada ya kupata Tuzo katika maonesho ya 14 ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mwanza. Kilele cha maonesho hayo kitakuwa tarehe 8 Septemba, 2019. Tuzo hizo ni vyeti na makombe kama mshindi wa kwanza katika kipengele cha Central and Local Governments, Departmenta and Exhibitors na pia mshindi wa ujumla kwa Waoneshaji wote (Overall Winner Exhibitors). Ushindi huo umetangazwa katika hafla za ufunguzi wa maonesho hayo tarehe 2 Septemba, 2019 kwenye viwanja vya Rocy City Mall, Mwanza na mgeni Rasmi alikuwa ni Bw. Edwin Rutageruka, Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE. Kauli mbiu ni ‘kuongeza ubunifu katika uzalishaji na biashara katika kukuza uchumi wa nchi yetu’.

 

Akielezea sababu za ushindi huo mnono, Bw. Lukwaro amesema ni ‘ubunifu katika kuandaa banda na kuonesha kwa vitendo mfano wa namna ambavyo mwekezaji anapata huduma/usaidizi wa kuanzisha mradi wake kutoka taasisi zaidi ya kumi sehemu/mahala pamoja (One Stop Facilitation Centre). Vilevile washiriki waliotembelea banda la TIC walielimishwa kinagaubaga juu ya masuala ya uwekezaji kutoka kwa timu ya wafanyakazi wenye ari. N kipekee kabisa safari hii timu imejipanga kushawishi wafanyabiashara na wawekezaji walio nje ya mfumo wa TIC ambao wanakidhi viwango vya kujisajiri na Kituo kujisajili. Hatua hii itawawezesha kutekeleza miradi yao huku wakipata usaidizi wa Serikali kupitia TIC ikiwamo vivutio vya kikodi na visivyo vya kikodi’.

 

Aidha, katika kuhakikisha kwamba TIC inafanikisha utekelezaji wa kauli mbiu ya maonesho, wawekezaji na wafanyabiashara wanahamasishwa kutumia/ kuwekeza kwenye ubunifu wanapokuwa wanatekeleza miradi yao. Jambo hili ni muhimu katika kufikia mafaniko makubwa ndani ya muda mfupi. Miradi inayonadiwa na Kituo inalenga sekta za Viwanda vya Ngozi na bidhaa za Ngozi; Viwanda vya kuchakata/kusindika mazao ya  kilimo, mifugo, misitu na uvuvi; Viwanda vya pamba na nguo; Viwanda vya madawa ya binadamu; Uanzishaji wa maeneo ya kanda maalumu wa SEZs / EPZs;  Viwanda vya kuunganisha magari na vipuri; Viwanda vya kutengeneza mafuta ya kula na Viwanda vya mabati na chuma/nondo kwa ajili ya ujenzi.

 

Pongezi za pekee pia ziwafikie timu ya TIC Kanda ya Ziwa katika maeonesho hayo Bi. Haigath Kitala Meneja wa Uhamasishaji Uwekezaji Ndani  (Makao Makuu Dar es Salaam), Linda Loomu (Afisa Uhamasishaji Uwekezaji (Mwanza), Sara Mwingira (Katibu Muhtasi, Mwanza), Afisa Ardhi na Afisa Biashara (Mkoa wa Mwanza).

Social Medias

Copyright ©2018 Tanzania Investment Centre.
All Rights Reserved.
Designed, Developed, and Maintained by Tanzania Investment Centre(TIC)