The United Republic of Tanzania

TANZANIA INVESTMENT CENTRE

Tanzania sio nchi pekee inayovutia wawekezaji duniani, tufanikishe uwekezaji .


 Juni, 2019: Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geoffrey Mwambe amefanya mazungumzo na  Mhe. Dkt. Ulisubisya Mpoki kenye ofisi za Mako makuu ya TIC Dar es Salaam. Dkt. Mpoki ameteuliwa hivi karibuni na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada.

Ujio wa Dkt. Mpoki TIC umekuja baada ya kuapishwa ili kubadilishana mawazo na uongozi kwa lengo la kupata mwelekeo/mwongozo zaidi wa masuala ya uwekezaji anapokusudia kwenda kutekeleza majukumu yake  nchini Canada.  Aidha Mhe. Balozi ametembelea Kituo ili  kupata taarifa na elimu zaidi juu ya namna ambavyo ofisi ya ubalozi wetu huko Canada inaweza kusaidiana na Kituo katika kuvutia, kuendesha na kusimamia masuala ya uwekezaji  kwa maslahi ya Taifa.

Mhe. Balozi ameahidi kufanya kazi karibu na Kituo ili kuhakikisha kwamba anapata  taarifa na miradi  ya sekta mbalimbali inayoendana na wakati kwa ajili ya kunadiwa  sambamba na kupata  taratibu za kuwekeza. Kipekee kabisa, Mhe. Balozi   ametoa wito/angalizo kwa taasisi zote zinazohusika na kusaidia wawekezaji kupata vibali/leseni/vyeti/miongozo ya kuwekeza nchini kuzingatia uharaka wa kutoa huduma/majibu husika badala ya kuchelewesha. Kufanya hivyo kutahamasisha na kuvutia zaidi wawekezaji badala ya  kuwachosha na majibu ya nenda rudi kwa muda mrefu bila kupata muafaka kwa wakati stahiki.

akifafanua Mhe. Balozi amesema, sasa ni wakati muafaka kwa viongozi wa Serikali wenye kutoa maamuzi kutimizaji wajibu kwa wakati na haraka ili kuwezesha/kufanikisha  uwekezaji  zaidi nchini kama Mhe. Rais Magufuli anavyohimiza. Tusiwe vikwazo /kuwakatisha tamaa wawekezaji kwa utoaji wa huduma zetu na kuwakimbizia nchi nyingine. Hii ni kutokana na ukweli kwamba Tanzania sio nchi pekee inayohitaji wawekezaji.

Naye Geoffrey Mwambe, pamoja na mambo mengine  amemweleza Mhe. Balozi kuwa TIC ina jukumu la kuinadi nchi kama sehemu nzuri ya kuwekeza kwa lengo la kuvutia wawekezaji wengi huku tukilenga kufanikisha utekelezaji wa dira ya nchi 2025. Kwa kuzingatia hilo, Mwambe amemweleza Mhe. Balozi kuwa nchi inahitaji wawekezaji kwa wingi kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Canada. Hivyo uteuzi wake kwenda nchini Canada Kituo kinachukulia kama fursa katika kuvutia wawekezaji wapya wenye nia ya kuwekeza kwenye sekta za kipaumbele.

Akifafanua Mwambe amesema ‘Kituo kina taarifa za makampuni yaliyowekeza nchini  kutoka Canada lakini bado juhudi zaidi zinahitajika na ushawishi ili kuhamasisha na kuvutia wawekezaji wengi zaidi. Mwambe pia ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha  wawekezaji kutoka Canada kuja kuwekeza kwenye maeneo ya viwanda, kilimo na kuongeza thamani, uvuvi na kuongeza thamani, kuunganisha magri, madini na kuongeza thamani, madawa  na vifaa tiba, ujenzi, hoteli, elimu, na mioundombinu’.

Mwisho, Kituo kimemkabidhi Mhe. Balozi mfuko wenye miongozo na taarifa mbalimbali ya namna ya kuwekeza Tanzania.

Social Medias

Copyright ©2018 Tanzania Investment Centre.
All Rights Reserved.
Designed, Developed, and Maintained by Tanzania Investment Centre(TIC)