The United Republic of Tanzania

TANZANIA INVESTMENT CENTREMdahalo wa kusikiliza changamoto za Wawekezaji ni hatua ya kutafuta ufumbuzi wa kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini. .


 

17 Aprili,2019: Mhe. Angellah Kairuki amekuwa Mgeni rasmi na Mwenyekiti kwenye mdahalo wa wawekezaji wa Kichina waliowekeza nchini. Mdahalo huo umefanyika Serena Hotel, Dar es Salaam na pia umehudhuriwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Inj. Stella Manyanya (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Damas Ndumbaro (Mb), Balozi China nchini Mhe. Wang Ke na Wakuu/ Wawakilishi wa Taasisi za Serikali zipatazo ishirini (20).

 

Lengo la mdahalo lilikuwa ni kusikiliza changamoto za biashara na uwekezaji kutoka kwa Wachina waliowekeza nchini ili kuzitolea majibu na ufafanuzi. Aidha mdahalo pia ulilenga kutoa elimu/ kuwakumbusha wawekezaji wa Kichina njia sahihi za kufuata na nyaraka za kuwasilisha wanapoomba kupata huduma husika ili waweze kupata vibali, leseni na vyeti vinavyohitajika kufanikisha uwekezaji wao hapa nchini bila usumbufu usiokuwa wa lazima.

 

Kwa upande wao wawekezaji wa Kichina, wameeleza changamoto zao na kupatiwa majawabu/ ufafanuzi  juu ya masuala mbalimbali jambo ambalo limewafurahisha. Majibu yametolewa na Wakuu/ Wataalamu wa Taasisi mbalimbali zinazohusika moja kwa moja kusaidia wawekezaji kuwekeza nchini.

 

Mwisho,Balozi wa China nchini ameipongeza Serikali kwa hatua hiyo ya kuitisha mdahalo ambao umewezesha kutoa ufafanuzi /majibu ya changamoto za wawekezaji kutoka China. Aidha Mhe. Balozi amehitimisha kwa kusema kuwa kusikiliza na kufafanua/kutoa majawabu ya changamoto za wawekezaji hao imekuwa ni hatua kubwa  na mchango katika kutafuta suluhu ya kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji si tu kwa Wachina bali pia na kwa wawekezaji wa nchi nyingine waliowekeza nchini. Ili kuleta ufanisi zaidi, imekubaliwa kuundwa kamati itakayofuatilia utekelezaji wa masuala yaliyokubaliwa kwa pamoja.

 

Mdahalo uliofanyika ni mwanzo na kati ya mikakati ya kutatua changamoto za wawekezaji nchini ambapo midahalo mingine ya aina hiyo itafuata kwa wawekezaji wa nchi nyingine zilizowekeza hapa nchini.

 

Social Medias

Copyright ©2018 Tanzania Investment Centre.
All Rights Reserved.
Designed, Developed, and Maintained by Tanzania Investment Centre(TIC)