The United Republic of Tanzania

TANZANIA INVESTMENT CENTRE

We have no plan and we have not thought of closing the industry in Tanzania, ‘DANGOTE'’ .


FEBRUARY, 2021; The management of Dangote Cement Factory in Tanzania  has spoken to the press conference to refute rumors circulating on social media that the factory wants to close its investment activities in the country. The CEO of Dangote Company Mr. Abdullah Baba has said the Dangote company exists, and has not considered leaving at all. So the information that appears on social media is not true and does not belong to the leadership of Dangote Factory.

 

"There are unofficial reports circulating online for some time now against the Dangote factory seeking closure, it should be noted that the information is not true it is a rumor so ignore it," said Baba.

 

Mr. Baba further clarified that, when Dangote Management wants to communicate with the public it uses the office system which includes convening meetings with the media with the aim of reaching out to the people accordingly. He said the factory is now more stable and continues with its production which has increased to 5,000 tons per day since they started using natural gas energy. Dangote are happy with the increase in production level as they are confident of the market for their products in and out of Tanzania.

 

On top of that, the Relationship Manager of Dangote Factory Mr. Siraji Nalikame said, Dangote Tanzania does not communicate with the public through social media but instead uses official procedures in reaching out to the public. When anything happens that they think is best for the public, they use official procedures to call the media and talk and not otherwise. So the information that has been coming out of social media is unofficial and has not been from Dangote's leadership.

 

Dangote Tanzania is proud of the good relations and close cooperation with the Government Authority at the District, Regional and the Ministry levels which has largely succeeded in solving the challenges that have been facing them.

 

"I would like to take this opportunity to once again inform the public that Dangote has no plans and has not considered leaving Tanzania. They will  exist and continue with their investments',said Nalikame.

 

Mr. Nalikame has also used the opportunity to invite other investors interested investing in Tanzania to approach the Tanzania Investment Center (TIC) which assists investors from the initial stages of registration to the implementation of the project through One Stop Facilitation Center.

 

 

HATUNA MPANGO NA HATUJAFIKIRIA KUFUNGA KIWANDA TANZANIA, ‘DANGOTE’

 

Februari,2021: Menejimenti ya Kiwanda cha Saruji cha Dangote Tanzania kilichopo Mkoani Mtwara imezungumza kwenye mkutano wa vyombo vya habari ili kukanusha taarifa za uvumi zinazoendelea kwenye mitandao ya kijamiii kwamba kiwanda hicho kinataka kufunga shughuli zake za uwekezaji hapa nchini.

 

 Katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Dangote nchini Bw. Abdullah Baba amesema kampuni ya Dangote ipo, na haijafikiria kuondoka hata kidogo. Hivyo taarifa zinazoonekana kwenye mitandao ya kijamii sio za kweli na sio za uongozi wa Kiwanda cha Dangote.

 

‘Kuna taarifa zisizo rasmi zinazosambaa mitandaoni kwa muda sasa dhidi ya kiwanda cha Dangote kutaka kufungwa, ifahamike kwamba taarifa hizo sio za kweli ni uvumi hivyo zipuuzeni,’ amesema Bw. Abdul.

 

Bw. Abdul amefafanua zaidi kwamba, Menejimenti ya Dangote inapotaka kuwasiliana na umma inatumia utaratibu wa ofisi  ambao ni pamoja na kuitisha mikutano na vyombo vya habari kwa lengo la kuwafikia wananchi ipasavyo. Amesema kiwanda kwa sasa kipo imara zaidi na kinaendelea na Uzalishaji wake ambao umeongezeka hadi kufikia tani 5000 kwa siku tangu walipoanza kutumia nishati ya Gesi asilia. Dangote wanafurahia kuongezeka kwa kiwango cha uzalishaji kwa kuwa wana uhakika wa soko la bidhaa zao ndani na nje ya Tanzania kutokana na ubora.

 

Aidha, Meneja wa Mahusiano wa Kiwanda cha Dangote Bw. Siraji Nalikame amesema, kampuni ya Dangote Tanzania haiwasiliani na Umma kupitia mitandao ya kijamii badala yake inatumia taratibu rasmi za kiofisi katika kuufikia Umma. Kunapotokea jambo lolote wanalodhani ni vema kuufikia Umma, wanatumia taratibu za kiofisi za kuita vyombo vya habari na kuzungumza na sio vinginevyo. Hivyo taarifa ambazo zimekuwa zikitoka kwenye mitandao ya kijamii sio rasmi na zimekuwa hazitokani na uongozi wa Dangote.

 

 Bw. Nalikame pia amesema, Dangote Tanzania inajivunia mahusiano mazuri  na ushirikiano wa karibu na Mamlaka ya Serikali katika ngazi ya Wilaa, Mkoa hadi Wizarani jambo ambalo limefanikisha kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili.

 

‘Nachukua fursa hii kwa mara nyingine kuutangazia Umma kuwa, Dangote haina mpango na haijafikiria kuondoka Tanzania ipo na itaendelea kuwepo’, amesema Bw. Nalikame.

 

Mwisho, Bw. Nalikame  ametumia furasa hiyo kuwakaribisha wawekezaji wengine wenye nia ya kuwekeza Tanzania kukaribia ili kufanikisha uwekezaji wao nchini. Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kupitia Mfumo wa Mahala Pamoja ’One Stop Facilitaion Centre’ kitawasaidia kuanzia hatua za awali  za usajili mpaka utekelezaji wa mradi husika.

Social Medias

Copyright ©2018 Tanzania Investment Centre.
All Rights Reserved.
Designed, Developed, and Maintained by Tanzania Investment Centre(TIC)